![]() |
| Usikubali ngono ikatishe maisha yako. Weka malengo, timiza ndoto zako na UCE |
KUWEKA NA KUTIMIZA MALENGO
- Maisha
yenye afya
- Mahusiano
yenye afya
- Kazi na
wajibu
- Kufanikiwa
zaidi katika maisha
- Kuboresha
mafanikio kiujumla
- Kuongeza
motisha ya kufanikiwa zaidi katika maisha
- Kuongeza
fahari na furaha katika mafanikio yako
- Kuongeza
kujiamini na kukua kwa utu wa mtu
- Kuondoa
mtazamo unaokurudisha nyuma na kukusababishia kukosa furaha
- Kupungua
kwa msongo na hali ya wasiwasi uliopindukia zaidi
- Unataka
kufanya nini na maisha yako?
- Unataka
kufanikisha nini?
| UCE team haifungwi na umbali, iwe mlimani, bondeni porini, tutakufikia kukuelimisha. Pichani ni Afisa uhamasishaji wa UCE Mr Mgina akitoa semina kwa wanafunzi wa Wasa Sekondari |
- Afya: Je unataka kuwa na afya ya aina gani kimwili,
kiakili, kijamii na kiroho?
- Mtazamo:
Upi mtazamo wako wa kimaisha?
- Kipaji /
karama: Je una kipaji gani?
- Elimu / Ujuzi:
Je ungependa kujiajiri au kuajiriwa?
- Familia: Je
ungependa kuwa mzazi wa aina gani?
- Fedha: Je
ungependa kuwa na kipato cha aina gani? Katika umri gani?
- Starehe: Ungependa
kuyafuraiaje maisha yako?
| Mratibu Mipango UCE Mr Lema , katika semina Ilula , ukanda wa Mazombe |
Aina / Eneo la
Lengo m.f. Afya n.k
|
Faida za Lengo
Husika
|
Mchakato /
Ufunguo
|
Muda
|
Rasilimali
|
Matokeo
|
Toa
maana ya lengo lako, liandike kutokana na mpangilio na kipaombele
|
Orodhesha
faida utakazopata kwa kufanikisha lengo lako,
Jambo
gani litakufanya uwe mwenye furaha?
|
Hatua
zipi unatakiwa kufuata ili kutimiza lengo lako,
Je
utaanza na hatua ipi?
|
Andika
muda wa kuanza na utakaohitajika katika kulitimiza lengo lako
|
Andika
mahitaji yanayohitaji-ka katika kulitimiza lengo
Je
utazipata wapi?
|
Umefanikisha
nini?
Wapi
umekwama, na zipi sababu za kufanikiwa au kukwama?
Je
lengo lako litaleta athari gani katika maisha ya sasa na yajayo?
|
- Kupanga malengo ya matokeo pasipo kupangilia
utekelezaji wake hatua kwa hatua
- Kupanga malengo yasiyo na uhalisia kwani hakuna
jitihada za kuyatimiza
- Kupanga malengo yasiyoleta changamoto wala
faida inayoonekana
- Kutokuwa na mpangilio wa lipi lianze na lipi
lifuate
- Kupanga malengo mengi kwa wakati mmoja
| Kicheko cha kiwango cha lami kwa mwanafunzi wa Nanenane sekondari Morogoro baada ya kufanya maamuzi ya kusubiri kwa kusaini kadi ya UCE. |
- Tafakari na jenga taswira ya maleongo yako
- Fikiria yapi yanaweza kukwamisha malengo yako
- Ainisha na bainisha mambo yatakayokusaidia
kutimiza malengo yako
- Pitia mara kwa mara malengo yako
- Jiwekee yapi ya kufanya na yasiyo ya kufanya
(Do’s and Don’ts)
- Jifunze kutawala muda wako vizuri (time
management) kwa kuoorodhesha yale yanayoiba au kupoteza muda wako
- Jifunze kutawala msongo katika hatua zote za malengo
yako
- Usiweke malengo madogo kwa kuhofia kushindwa
- Ni vyema kujua kushindwa kutimiza lengo
haijalishi sana iwapo kuna funzo umejifunza katika hilo lengo
- Kumbuka malengo yako yawe kwa yale unayotaka
kufanikisha katika maisha yako kwani mafanikio huja pale unapofanya kwa
ajili ya ustawi wako
| Wanafunzi wa Mbalali sekondari mkoani Mbeya wakifurahia maamuzi yao ya kusubiri. INAWEZEKANA |
![]() |
| Karibu UCE Taanzania ujifunze mengi juu ya kulinda na kuimarisha afya |




